KUJILINDA DHIDI YA KURUDI NYUMA KUTOKA KWA KRISTO
Inawezekana kwa Wakristo kuwa wanazarawu mambo ya kiroho, kushikiliwa nakutokuomba, kupitia siku yote bila kutafuta Neno la Mungu. Naam, Biblia inaonya kwa wazi kwamba inawezekana kwa waumini wenye kujitolea kujitowa kwa Kristo na inatoa maonyo yenye nguvu juu ya kujilinda usingizi katika saa ya usiku wa manane: "Kwa hiyo imetupasa kuyaangilia zaidi ya hayo yaliosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?" (Waebrania 2:1-3).