ONGEZEKO LA UWEPO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu anafanya jambo jipya katika kanisa lake leo. Kazi hii kubwa ya Roho haiwezi kupatikana katika eneo moja. Inatokea ulimwenguni pote, ndio, hauitaji kufanya safari ya mbali ili uyikumbatiye. Hakika, "kitu kipya" cha Mungu kinaweza kuwa karibu kama kanisa lilivyo karibu.

KUPENDANA KWA UJASILI KAMA YESU ALIVYOFANYA

Gary Wilkerson

Tunapochunguza maisha yetu kama wafuasi wa Yesu, wengi wetu hafwaati mfano wa Agano Jipya. Kristo aliwatuma wanafunzi wake kumi na wawili kuitangaza habari njema, kuponya wagonjwa, na kuwa tayari vyombo vya kuleta ufalme wake duniani (angalia Marko 16:15-18). Baadaye, aliwatuma wanafunzi sabini na maagizo sawa (angalia Luka 10:1-16). Aliwaambia kila mmoja wa makundi haya, "Kila kitu niliowafundisha kufanya - kuhubiri injili, kuponya wagonjwa na kuleta ndani ya ufalme wangu - munapaswa kufanya hayo kwa jina langu. Sasa nenda ulimwenguni pote na mufanye kama nilivyoamuru."

UPWEKE UKO MAHALI POTE

Nicky Cruz

Tunahitaji kutofautisha kati ya kuwa mwenyewe, upweke na kutengwa. Kuwa mwenyewe, ni hali ya kujitenga na watu wengine. Wakati mwingine familia, marafiki na watu wengine kwa kutopatikanan mbele yetu, lakini tu kwa sababu sisi tuko wenyewe haimaanishi sisi tuko kwenye upweke. Tunachukua tu nyakati hizi kwa kuzingatia na kutambua kuwa maisha haiwezi kujazwa na watu daima.

KUJIANDAA KWA SIKU ZIJAZO

David Wilkerson (1931-2011)

"Siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku" (2 Petro 3:10). Mungu hutumia watumishi waaminifu - wakati mwingine wale wenye vurugu za kitaifa na wakati mwingine wanyenyekevu, wasiojulikana, walinzi wa siri - kutoa maneno yake ya onyo. Ni wale tu ambao hawapendi dunia hamu sana ya kuja kwa Bwana kwa kuwa atawalete ujumbe wa kweli katika mioyo yao.

​MUNGU AMESHIKILIA NENO LAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Ujasiri katika sala hutoka kwa kuwa na ujuzi wa kitu kinachoitwa "kushikilia kipaumbele." Ikiwa unaweza kuelewa ukweli huu, utabadili milele namna yakuomba. Mfano ni "kesi iliyotangulia" ambayo hutumika kama mfano katika kesi zifuatazo. Na "kushikilia kipaumbele" ni uamuzi wa kisheria uliofanywa zamani ambao unakuwa utawala wa mamlaka kwa kesi sawa za baadaye. Kwa majaji, hii inamaanisha kusimamia uamuzi uliofanywa tayari.

UNAKWENDA WAPI UNAPOKABILIWA NA SHIDA?

David Wilkerson (1931-2011)

Unaweza kufurahia msimu wa nyakati nzuri sasa - hakuna shida kubwa, majaribio ya kukata tamaa au maumivu makubwa. Ninamshukuru Bwana kwa kutoa nyakati hizo katika maisha ya watoto wake. Lakini tunajua kutoka kwa Maandiko kuwa dhoruba na majaribu makubwa hatimaye huja kwa wote ambao wametowa kwa ukweli kila kitu kwa Kristo. "Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya kutoka yote" (Zaburi 34:19).

JE, UNAHITAJI NGUVU?

Gary Wilkerson

"Je! Kufunga ninayochagua; siyo yamna hii? kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza Kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira" (Isaya 58:6). Mungu anasema kuwa kufunga anayechagua, huanza ndani ya mioyo yetu wenyewe. Tunapaswa kuwa namsimamo wenyewe wa kupokea kitu kisicho cha kawaida kutoka kwa Mungu - uhuru kutoka kwenye ukandamizaji na utumwa wa kila aina.

KWA WOTE WALIO MBALI

Carter Conlon

"Ndipo Petro akawaambia," Tubuni, na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi; na mtapokea kipawa ach Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu" (Matendo 2:38-39).

TUNAMTUMIKIA MFALME MWENYE HAKI

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana anatawala juu ya viumbe vyote kwa utukufu na nguvu. Sheria zake zinatawala ulimwengu wote - kila asili, taifa lote, na mambo yote ya wanadamu. Anatawala juu ya bahari, sayari, miili ya mbinguni na harakati zao zote.

"Atawala kwa uweza wake milele; Macho yake yanaangalia mataifa" (Zaburi 66:7). "Bwana hutawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika, Amejifunga kwa nguvu ... Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; Wewe ndiwe tangu milele ... Ushuhuda wako ni uhakika sana" (Zaburi 93:1-2, 5).