BABA YAKO ANASHIKILIA AHADI ZAKE
Gethsemane ilikuwa ni bustani ambako Yesu alikwenda kuomba wakati kesi yake ilipoibuka na kikombe chake kilipomshinda. Ndio pale aliliaa kwa huzuni zake za kina mbele ya Baba. Na pia ni pale ambapo alishinda vita juu ya kila uovu na nguvu.
Wakristo wengine leo wanasema, "Kizazi chetu sio chenye machozi. Tumeitwa kusherehekea na kuamuru kuchukua kila kitu kwa imani. Tunaweza kusema Neno na kila mlima ukahamishwa. Tunapaswa tu kutafakari juu ya uzuri wa Mungu." Hiyo ndio mkao wa kanisa la kisasa la mafanikio.