Body

Swahili Devotionals

KATIKA SAA HII YA MWISHO

David Wilkerson (1931-2011)

Petro na wanafunzi walipoona kile kilichofanyika siku ya Pentekoste, Petro mara moja akasimama akasema, "Lakini jambo hili lililonenwa na nabii Yoeli ... 'Naamu, na siku hizoNitaimwaga Roho yangu'" (Matendo 2:16, 18). Vivyo hivyo, tunaweza kuona katika Maandiko yale ambayo Roho Mtakatifu anafanya katika siku hizi za mwisho - kwa kweli, katika saa hii ya mwisho.

Nabii Malaki hutoa unabii wa mara mbili: Kwanza, anazungumza na ulimwengu usiomcha Mungu, wa kivitu tu na kimwili, ulimwengu ulioharibika sana. Na pili, anaongea na wale wanaompenda na kumwogopa Bwana.

HALI ZISIOWEZEKANA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alikuwa akihudumia umati mkubwa wakati watu walianza kuwa na njaa. Akamchukua Filipo mwanafunzi wake kando akamwuliza swali muhimu: "Basi Yesu alipoinua macho yake, akaona watu wengi wakimwendea, akamwambia Filipo, Tutununue wapi mikate, ili hawa wapate kula?" Yohana 6:5-6).

UWEPO WA MUNGU NI TOFAUTI

Gary Wilkerson

Tunapomtazama Ibrahimu katika Agano la Kale, tunashuhudia mtu ambaye uhai wake ulijaa kuja mbele ya Mungu hata hata wajumbe waliokuwa karibu naye walitambua tofauti kati ya maisha yao na yake: "Abimeleki ... alizungumza na Abrahamu, akisema, 'Mungu yu pamoja nawe katika yote unayoyafanya" (Mwanzo 21:22). Mfalme huyu mpagani alikuwa akisema, "Kuna kitu tofauti na wewe, Ibrahimu. Hakika Mungu yu pamoja nawe popote unapoenda."

KUKABILIYANA NA ADUI KWA UJASIRI

Nicky Cruz

Ikiwa tunaliamini au la, ni kweli kwamba Shetani yuko kwenye ujumbe - ujumbe ulivyo rahisi kama kwa nia moja. Yeye yuko nje ili aibe nia yetu na ameamua kuitimiza. Fikiria jinsi anaweza kuwa na ufanisi kama anaweza kutekeleza kazi hii moja - hii moja ya kutafuta. Kitu hiki anachohitaji sana kufikia.

KIVULI CHA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Yeremia nabii asiye na hofu, mhubiri mwenye nguvu wa utakatifu na toba, alikuwa na akili ya Mungu na akutembeya katika hofu ya Bwana. Hata hivyo, tunaposoma Yeremia 20, tunamwona huyu mtu mukubwa anayesumbuliwa na kivuli cha imani.

MUNGU HUWAPA NGUVU WALE WALIO DHAIFU

David Wilkerson (1931-2011)

"Kama Mungu alivyomgaia kila mtu kiasi cha imani" (Warumi 12:3). Waumini wote wanapewa sehemu au shahada ya imani na sehemu hiyo lazima iwe imejengwa kuwa imani isiyoweza kutingizika, na isiyo yumbayumba. Je! Hii inatokeaje? Kama imani inakua, inaimarishwa kwa njia moja tu: kupitia kusikia na kuamini Neno la Mungu.

FARAJA ISIYO YA KAWAIDA

David Wilkerson (1931-2011)

"Na ahimidiwe ... Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote, ili nasi tuweze kuwafariji nawale walio katika dhiki ya namna yote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu" (2 Wakorintho 1:3-4). Kote duniani, watu wanapitia mateso na majaribio, na Bwana ameahidi kutufariji ndani ya hao. Ona kwamba hakuna kitu kinachosemwa hapa juu ya ukombozi kutoka kwenye vita; tunaambiwa tu kwamba Roho Mtakatifu anatupa faraja ya kuvumilia na kukaa imara katika jaribio letu.

YESU ANATUOMBEA

David Wilkerson (1931-2011)

Siku ya Pasaka, Yesu aligeuka kwa mwanafunzi mwenye ujasiri Petro na kufunua, "Petro, Shetani ametaka mimi kukupeleka kwa yeye ili aisumbue maisha yako."

"Bwana akasema, 'Simoni, Simoni! Tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakaporudi Kwangu, waimarishe ndugu zako." Naye akamwambia,"Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi nitayari kwenda gerezani au hata kifoni." Kisha akasema,"Nakwambia, Petro, jogoo hatawika leo kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijuwi" (Luka 22:31-34).

YESU HAWEZI KUSHINDWA KAMWE

Gary Wilkerson

"Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja name popote nilipo, wapate kuona utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu" (Yohana 17:24, msisitizo wangu). Yesu aliwaombea wanafunzi wake - na hilo linajumuisha sisi. Alimwomba Baba ili tuweze kuona utukufu wake, inamaanisha kwamba tunamjua.

SALA ILIYOONGOZWA NA ROHO YA MUNGU

Jim Cymbala

Paulo aliwaambia waefeso "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho" (Waefeso 6:18). Nini maneno ya kuvutia na picha ya maneno - kuomba katika Roho. Omba katika Roho, omba katika, kupitia, na kwa Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu mwenyewe!

Kwa kuongeza mufano huu katika Waefeso, kuna mengi: "Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia" (1 Wakorintho 14:15). Juwa kwamba Paulo huomba si kwa mawazo yake tu bali pia kwa roho yake, alichochewa na kuongozwa na Roho wa Mungu.