NI NINI KINACHOZUIA KAZI YA MUNGU NDANI YETU?
"Basi nitasifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili nguvu za Kristo ziwe juu yangu" (2 Wakorintho 12:9). Mtume Paulo alikua dhaifu kwa sababu ya shida na dhiki lakini wakati alipotiwa chini, hakukata tamaa. Alifurahi katika mchakato wa kuwa dhaifu kwa sababu ilikuwa ni siri ya nguvu zake na Kristo, na kutokana na udhaifu huo akawa na nguvu.