Body

Swahili Devotionals

ROHO YA MUNGU HAYIJAISHA KAMWE

David Wilkerson (1931-2011)

Ikiwa tunaishi kwa imani, hatutaogopa kwa wakati ujao wa kanisa la Mungu. "Juu ya mwamba huu nitaijenga kanisa langu, na milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathayo 16:18). Dhamira hii kutoka kwa Yesu imesisitiza imani ya vizazi na ina maana ya kutuunga mkono sasa katika kizazi hiki.

WATU WENYE KUTOSHEREZA

David Wilkerson (1931-2011)

Mtume Paulo aliandika, "Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi ni watoto wa Mungu" (Warumi 8:16). Maneno "watoto wa Mungu" mara nyingi hutumiwa kwa kuelezea waumini, lakini maneno yanaweza kutumiwa pia kwa uhakika, kwa ufahamu mdogo wa nguvu na kina cha maana yake ya kweli.

Kuwa mtoto wa Mungu inamaanisha tu kuwa mtegemezi wa Mungu; yaani, "asiyeweza kuwepo au kufanya kazi bila msaada kutoka kwa Mungu." Mtoto wa Mungu anajua hawezi kudhibiti maisha yake bila msaada wa kila siku wa Bwana.

FUNGA MLANGO

David Wilkerson (1931-2011)

Katikati ya muda wa kuchangamka na machafuko, watu wa Mungu wanajibuje? Ikiwa umemkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako, hauhitaji kamwe hofu. Wale ambao wako ndani ya Kristo wanahifadhiwa milele na damu ambayo Yesu alimwanga kwa ajili yao na ukweli huu ni jiwe kuu la imani yetu. Itaamua kila kitu tunachofikiri na kila tunachofanya bila kujali kinachoendelea kote kwetu.

HATA KWENYE SIKU YAKO MBAYA ZAIDI

Gary Wilkerson

Mtakatifu na kupakwa mafuta- haya ni mambo mawili muhimu ya maisha ya Yesu yanatakiwa kuwa sehemu ya maisha yetu pia. Tumeitwa kuwa watakatifu na watiwa mafuta lakini Wakristo wengine wanaweza kutishwa na hili. "Ninaishi maisha ya kimaadili na ninafanya kadili ninavyoweza ili niwe mtu wa Mungu - lakini mtakatifu? Na kupakwa mafuta? Je, hilo linawezaje kutokea, kwa kuzingatia kushindwa kwangu kwote?"

MUNGU HUTUMIA KITU KISICHO KAMILIFU

Jim Cymbala

Kwa kawaida, Mungu anapenda kuchagua watu wasiopendeza, wasiofundishwa, na wasio wakamilifu kutekeleza mambo ya kushangaza. Ibrahimu alidanganya wakati alishinikizwa, Musa alimuua mtu kabla ya kuwa mkombozi wa Israeli, familia ya Mfalme Daudi ilimutenga ili awe tu mvulana mchungaji, na mtume Petro alikuwa mvuvi ambaye hakuwa na mafunzo rasmi ya kidini.

KUTENDA KATIKA HOFU

David Wilkerson (1931-2011)

"[Yesu] hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutoamini" (Mathayo 13:58). Kutoamini kila wakati kuzuia utimilifu wa ufunuo wa Mungu na baraka, na Maandiko huonyesha wazi hilo kwamba Mungu hapende hilo hata kidogo. Anatupatia mfano wa jambo hili katika hadithi ya Mfalme Asa, mfalme mwenye haki na kizazi cha Daudi ambaye alitawala juu ya Yuda (soma akaunti katika 2 Mambo ya Nyakati 14 hadi 16).

HATARI KATIKA ULIMWENGU

David Wilkerson (1931-2011)

Sauti nyingi kanisa leo zinasema Wakristo wanapaswa kuonyesha aina mpya ya upendo. Wanasema juu ya upendo ambao ukweli wa kibiblia unapaswa kuendana na nyakati. Kulingana na injili yao, hakuna mabadiliko muhimu ya kibinafsi wakati mtu anapokubali Kristo. Hakika, hakuna toba inahitajika. Badala yake, lengo la kuwasilisha injili hii ni kuvunja tu kizuizi chochote kinachoweza kuonekana kuwa kikwazo ili mtu wa Kristo akubaliwe.

KUCHUKIWA BILA SABABU

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alisema alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea. Huyu alikuwa ule Mmoja aliye na uwezo wa kushinda upepo na mawimbi, lakini alikuja kama mtumishi mnyenyekevu. Injili zinatuambia kwamba alisikiliza watu kwa uvumilivu kilio chao. Watu wengi walimsihi Kristo kuwaokoa kutokana na mateso yao na alikutana na mahitaji yao. Aliwaponya wagonjwa, akafungua macho ya kipofu, masikio ya viziwi yaliyozibwa, akafunguwa ndimi zenye kufungwa, na akafanya walemavu kutembea. Yesu aliwaweka huru mateka kutoka kila aina ya utumwa - hata alifufua wafu.

JE! WEWE UMEZIDIWA NA HOFU?

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati hofu yetu imezidi, tunapaswa kujikumbusha jinsi Mungu wetu ni mkuu. Tunahitaji kukumbuka utoaji wake mkubwa kwa wale ambao waliomtegemea, na kudai nguvu za ajabu sawa kwa majaribio ya kisasa. Hofu haiwezi kupinga mtumishi yeyote ambaye ana maono ya ukuu wa Mungu na utukufu.