HATA KWENYE SIKU YAKO MBAYA ZAIDI
Mtakatifu na kupakwa mafuta- haya ni mambo mawili muhimu ya maisha ya Yesu yanatakiwa kuwa sehemu ya maisha yetu pia. Tumeitwa kuwa watakatifu na watiwa mafuta lakini Wakristo wengine wanaweza kutishwa na hili. "Ninaishi maisha ya kimaadili na ninafanya kadili ninavyoweza ili niwe mtu wa Mungu - lakini mtakatifu? Na kupakwa mafuta? Je, hilo linawezaje kutokea, kwa kuzingatia kushindwa kwangu kwote?"