Body

Swahili Devotionals

JE, UNAHITAJI NGUVU?

Gary Wilkerson

"Je! Kufunga ninayochagua; siyo yamna hii? kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza Kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira" (Isaya 58:6). Mungu anasema kuwa kufunga anayechagua, huanza ndani ya mioyo yetu wenyewe. Tunapaswa kuwa namsimamo wenyewe wa kupokea kitu kisicho cha kawaida kutoka kwa Mungu - uhuru kutoka kwenye ukandamizaji na utumwa wa kila aina.

KWA WOTE WALIO MBALI

Carter Conlon

"Ndipo Petro akawaambia," Tubuni, na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi; na mtapokea kipawa ach Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu" (Matendo 2:38-39).

TUNAMTUMIKIA MFALME MWENYE HAKI

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana anatawala juu ya viumbe vyote kwa utukufu na nguvu. Sheria zake zinatawala ulimwengu wote - kila asili, taifa lote, na mambo yote ya wanadamu. Anatawala juu ya bahari, sayari, miili ya mbinguni na harakati zao zote.

"Atawala kwa uweza wake milele; Macho yake yanaangalia mataifa" (Zaburi 66:7). "Bwana hutawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika, Amejifunga kwa nguvu ... Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; Wewe ndiwe tangu milele ... Ushuhuda wako ni uhakika sana" (Zaburi 93:1-2, 5).

​UPENDO WA MUNGU NI MKUBWA ZAIDI

David Wilkerson (1931-2011)

Baba yetu wa mbinguni anataka tuwe na uhakika wa kudumu kuhusu upendo wake. Yesu aliweka tatizo la dhambi zetu huko Kalvari na hata ingawa sisi wakati mwingine tunashindwa, Roho Mtakatifu anatukumbusha daima huruma ya Baba. Tunapozingatia dhambi zetu, tunapoteza kila kitu ambacho Mungu anataka zaidi: "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana yeye anayekuja kwa Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba Yeye huwapa thawabu wale wamutafutao" (Waebrania 11:6).

TUTAMUONA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

Mbinguni! Ahadi ya mbinguni ni msingi wa injili, lakini hatusikii mengi juu ya somo hili la furaha siku hizi. Kwa kweli, Biblia haisemi mengi kuhusu mbingu inavyofanana. Yesu hakuketi pamoja na wanafunzi na kuelezea utukufu na heshima vya mbinguni. Alimwambia mwizi msalabani, "Leo utakuwa pamoja nami katika Paradiso," lakini hakuielezea (Luka 23:43).

​UTEUZI WA KIMUNGU

Gary Wilkerson

"Mthiopiya, towashi ... alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi katika gari lake, na alikuwa akisoma nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, "Sogea karibu na gari hili" (Matendo 8:27-29).

Mtiopiya huyo, ambaye alikuwa mwekahazina wa Kandake, malkia wa Ethiopiya, alikuwa akienda hekalu huko Yerusalemu kuabudu, akiangalia kuingia katika njia mpya ya kuishi. Kupitia njia yote aliendelea kutafuta, na alikuwa akiketi karibu na barabara, akiisoma Maandiko katika mkokote wake.

TAHADHARI DHIDI YA KUSHINDWA KUOMBA​

Jim Cymbala

Kama Wakristo, tunahusika katika vita vya kiroho kama wajumbe binafsi wa Shetani wanapigana na roho zetu. Ingawa tunapaswa kupigana kila siku nguvu hizi zisizoonekana, Mungu ametupa silaha za kiroho - ngao ya imani, kofia ya wokovu, ngao ya kifuani cha haki, na kadhalika.

"Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya kuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho" (Waefeso 6:11-12).

KUSHINDA MBEGU ZA MASHAKA

David Wilkerson (1931-2011)

Yohana Mbatizaji alikuwa mtu wa Neno. Alitumia maisha yake yote akijifunza maandiko mahari pa upeke na kutafakari juu ya sheria. Alimwambia Yesu na kusema, "Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu" (Yohana 1:29). Alimwona Roho Mtakatifu akishuka juu ya Kristo kama njiwa, na akasikia sauti ya Baba ikumtangaza Yesu kuwa Mwana wake wa kipekee. Hata hivyo, Yohana alijikuta gerezani, huduma yake yenye nguvu, iliyotiwa mafuta imefupishwa na Mfalme Mwovu Herode (ona Luka 3:19-20). Sasa umati wa watu ambao ulikuwa unamfuata Yohana ulikuwa wakaondoka - "sauti ya mtu inayolilia jangwani" ikasimama.