MASAA YA UDHAIFU MKUBWA ZAIDI
"Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, siku zote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema maombi yangu kwa furaha, kwa sababu ya ushirikiano wenu katika kuineza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata hivi sasa. Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi nzuri ndani yenu ataimaliza hata siku ya Yesu Kristo; vile vile kama ilivyo wajibu wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kutetea Injili na kuithisbitisha, ninyi nyote mmeshirikiana name neema hii.