UTUKUFU WA KRISTO NDANI YETU

David Wilkerson (1931-2011)

"[Musa] akasema," Tafadhali, nionyeshe utukufu wako. "Kisha akasema," Nitapitisha wema Wangu wote mbele yako, nami nitatangaza jina la Bwana mbele yako. ... Itakuwa hivyo, wakati utukufu Wangu unapita, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na nitakufunika kwa mkono Wangu hata nitapokuwa nimekwisha kupita. Ndipo nitauondoa mkono wangu, nawe utaniona mgongoni mwangu; lakini uso Wangu hautaonekana ” (Kutoka 33:18-19, 22-23).

KUZAA MATUNDA AMBAYO YANAENDELEA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alisema, "Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mtunza shamba wa mizabibu. Kila tawi ndani Yangu lisilozaa matunda Yeye huliondoa; na kila tawi linalozaa matunda Yeye hulisafisha, ili lizidi kuzaa matunda… Mtu yeyote asikiaye ndani Yangu, hutupwa nje kama tawi na kukauka; na watu huyakusanya na kuyatupa motoni na kuchomwa” (Yohana 15:1-2, 6).

MAISHA YA UTAKATIFU NA SHUKRANI

David Wilkerson (1931-2011)

"Furahi siku zote, ombeni bila kukoma" (1 Wathesalonike 5:16-17). Watoto wa Mungu wanapaswa kufanya kuwa jambo la dhamiri kufurahiya kwake wakati wote na kila hali. Kufurahi sio chaguo letu; ni amri ya Mungu! Ikiwa tunachukua maneno haya kama chaguo, tunadhoofisha umuhimu wa Mungu kwetu.

Mpaka Mungu anayo furaha yetu, kwa kweli hana mioyo yetu. Kuna hatua tatu ambazo zitatusaidia kudumisha msimamo wa kufurahi katika Mwokozi wetu:

JE! WEWE UNASHIRIKI MALANYINGI MEZA YA BWANA?

David Wilkerson (1931-2011)

Daudi alisema juu ya Mola wake, "Waandaa meza mbele yangu, machoni ya maadui zangu" (Zaburi 23:5). Yesu alisema, "Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu" (Luka 22:29-30).

Jambo moja ambalo Bwana wetu anatafuta zaidi kutoka kwa watumishi wake, wahudumu na wachungaji ni kushirika mezani mwake. Umoja wakuzunguka meza yake ya mbinguni - mahali na wakati wa urafiki na kumjia kwake kila wakati kwa chakula, nguvu, hekima na ushirika.

KITU KILICHOONGEZWA KATIKA MOYO ULIOGEUKA

Gary Wilkerson

"Mwana- sharia mmoja ilisimama ili amjaribu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?" (Luka 10:25). Waandishi na Mafarisayo walikuwa wamekutana na Yesu, na kutowa changamoto kwa mamlaka yake mara nyingi lakini sasa mwana- sheria alimwendea, labda mtu aliyetumwa nao. Wana-sheria wamefunzwa vizuri katika sanaa ya mijadala na bila shaka huyu pia alikuwa na sifa nzuri katika sheria za Agano la Kale. Labda alitarajia Yesu aanze kurudia baadhi ya sheria kuhusu Sabato, kuosha mikono, chakula safi na chafu. Sheria nyingi! Na ni ipi inayoongoza kwenye uzima wa milele?

UAMSHO NYUMBANI KWAKO

David Wilkerson (1931-2011)

Msingi halisi wa nyumba ya Kikristo unatikiswa, matokeo ya moja kwa moja ya kuharibika kwa maadili na kiroho katika jamii yetu. Kwenye kitabu cha Matendo tunasoma juu ya muujiza mtukufu katika nyumba ya Kornelio - mabadiliko ambayo yalitokea kwa sababu mtu mmoja aliamua kuiona familia yake ikiokolewa.

JE! UNAAMINI ULINDAJI WA MUNGU?

David Wilkerson (1931-2011)

Kuna wakati kunaonekana kama Mungu hajajidhihirisha - wakati watu wake wameachwa kwa aibu na kukata tamaa - lakini hadithi kamili bado haijaambiwa. Katika Bibilia yote Mungu amekuwa na watu ambao imani kama-marumaru ilithibitisha uaminifu wake wakati wa nyakati ngumu zaidi. Watumishi hawa, bila woga, walimuachia Bwana kutenda.

USIOGOPE KILE UNAONA

David Wilkerson (1931-2011)

"Maana mikono ya waovu itavunjika, lakini BWANA huwasaidia wenye haki ... Hawataaibika wakati wa ubaya" (Zaburi 37:17, 19). Utabiri huu wa kushangaza kwa watu wa Mungu unatimizwa mbele ya macho yetu. Zaburi ya 37 inatuambia kwamba Bwana anainuka kuchukua hatua dhidi ya jamii ambayo dhambi zawo zimefika hadi mbinguni. Ndio Zaburi hii hiyo ni mojawapo ya tumaini kubwa, iliyo na ahadi ya ajabu kwa wale wanaomtegemea kabisa Bwana.

NJAA YA NAFSI

David Wilkerson (1931-2011)

Kuna njaa mbaya ya kutisha katika nchi hii leo. Sio njaa ya chakula bali ya hitaji la wanadamu. Watu wengi sana wamekosa upendo na ushikamano; kwa amani na kuridhika; kwa kusudi na kutimiza. Kwa kweli neno la njaa linamaanisha" uhaba mkubwa, njaa isiyokamilika, njaa ya aina yoyote." Hiyo inaelezea vizuri utupu ambao wengi wanapata leo.