JE! WEWE UKO SHAHIDI KATIKA JIJI LAKO?
Mara nyingi tunatarajia Mungu kutembea katika moja wapo ya njia mbili: ama kwa kumiminwa kimaajabu kwa Roho wake Mtakatifu ili kufagia umati katika ufalme wake, au kwa kutuma hukumu kuwaleta watu kwa magoti yao au hata kuwaangamiza. Lakini, wapenzi, hiyo sio njia ya Mungu ya kubadilisha mambo katika siku hizi mbaya. Njia yake ya kujenga magofu kila mara imekuwa ni kutumia wanaume na wanawake wa kawaida ambao amewagusa. Na yeye hufanya hivyo kwa kuwajaza Roho wake Mtakatifu na kuwatuma kwenye vita wakiwa na imani kubwa na nguvu! "Wote walijazwa na Roho Mtakatifu" (Matendo 2:4).