KUPENDA WENGINE KWAREJESHA
"[Yesu] alichukua kitambaa, akijifunga kiunoni. Kisha akatia maji ndani ya beseni na kuanza kuosha miguu ya wanafunzi, na kuipangusha kwa kutumia kile kitambaa alichojifunga” (Yohana 13:4-5). Wakristo wengine wanaojitolea hufuata mfano huu na hufanya huduma ya "kuosha miguu". Ingawa hii ni ya kufurahisha, kuna maana zaidi ya kujifunza kutoka kwa tendo hili. Kwa kweli, baada ya Yesu kuosha miguu ya wanafunzi wake, aliwauliza, "Je! Mmeelewa hayo niliyowatendea?" (13:12).