KAZI YA YESU MBELE YA KITI CHA ENZI
Bibilia inatuambia kwamba wakati Kristo alipanda mbinguni, alichukua huduma ya Kuhani Mkuu kwa wote wanaokuja kwake kwa imani. "Lakini Yeye, kwa sababu Anaendelea milele, ana ukuhani usiobadilika" (Waebrania 7:24). Yesu habadiliki - yeye yule jana, leo hata milele! Wakati utaendelea kuishi, atakuwa Kuhani wako Mkuu mbinguni, akiomba kwa niaba yako.
Yesu ameketi mkono wa kulia wa Baba, katika kiti cha enzi: "Tunaye Kuhani Mkuu wa namna hii, ambaye ameketi mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni" (Waebrania 8:1). Kuhani wetu Mkuu ana nguvu na mamlaka kwa amri yake.