Body

Swahili Devotionals

DARAJA KATI YA DUNIA NA MBINGU

David Wilkerson (1931-2011)

Wachungaji walipokuwa wakitazama juu ya mtoto huyo wakiwa ndani ya lango, waliona Mwokozi ambaye atakomboa wanadamu wote. Wale watu wenye busara walipomwona, waliona Mfalme ambaye angeshinda kifo. Na manabii walipoangalia mbele, walimwona Msimamizi ambaye angefungua milango ya gereza, afungue minyororo, na aachilie huru mateka. Wote walikuwa na maono yao ya Yesu ni nani na kwanini alifika.

HUPATIKANA KWA NEEMA YA MUNGU

Gary Wilkerson

"Mwezi wa sita Malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda katika mji wa Galilaya uitwao Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliochumbiwa na mtu ambaye jina lake ni Yosefu, wa nyumba ya Daudi. Na jina la bikira huyo alikuwa Mariamu. Akaingia nyumbani kwake, akamwambia, Salamu, ewe mpendwa, Bwana yu pamoja nawe! (Luka 1:26-28).

Kisha malaika akatangaza ajabu: "Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kutoka kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba katika tumbo lako na kuzaa mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi” (1:30-32).

AMANI KUPITIA TOBA

David Wilkerson (1931-2011)

"Nilikujulisha zambi yangu, na wala sikuuficha uovu wangu. Nilisema, Nitayakiri makosa yangu kwa Bwana,' na Wewe ukanisamehe maovu ya dhambi yangu” (Zaburi 32:5).

Daudi alikuwa mtu anayejua jinsi ya kutubu. Aligundua moyo wake kila wakati mbele za Mungu na alikuwa na haraka ya kulia, "Nimefanya dhambi, Bwana. Ninahitaji maombi."

JE! UNAZUBAA KATIKA IBADA?

David Wilkerson (1931-2011)

Ninataka kuzungumza nawe juu ya usumbufu wa akili wakati wa sala na kuachwa kwa ibada - haswa katika nyumba ya Mungu. Yesu aliwaita watu wanafiki ambao walikuja mbele Yake kwa maneno ya sifa, lakini akili zao na mioyo yao zilikuwa kwenye shuguli nyengine. Alizungumza nao moja kwa moja, akisema, "Unanipa kinywa chako na midomo yako - lakini akili yako iko mahali pengine. Moyo wako hauko karibu na Mimi!"

KUFURAHIA KATIKA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Maombi yanayompendeza Mungu ni rahisi sana na rahisi kuelewa. Wanafunzi wakamwambia Yesu, "Bwana, tufundishe kuomba" (Luka 11:1). Ombi hili linaonyesha hamu ya dhati ya kujifunza kusali kwa njia inayompendeza Bwana.

KUMRUHUSU MUNGU AKUPONYE KUVUNJIKA KWA MOYO WAKO

Gary Wilkerson

Yerusalemu ni ishara ya mji wa Mungu, au makazi ya Mungu. Kuunda tena kuta ilikuwa muhimu kwa sababu ilikuwa ishara kwa maadui wa Israeli, ilionyesha Mungu alikuwa na watu wake, na kufunua baraka zake.

Wakati Nehemia aliposikia kwamba kuta za Yerusalemu zilikuwa zimebomolewa zaidi ya nusu-karne baada ya kukamilika kwa ujenzi wa hekalu, "akaketi, akalia, na kuomboleza kwa siku nyingi" (Nehemia 1:4). Kisha akafunga na kuomba wakati anaandaa mpango wa kurekebisha hali hiyo.