KUENDELEZA TABIA YA MAOMBI
"Bali wewe unapoomba, ingia chumbani kwako, na ukisha kufunga mlango wako, omba kwa Baba yako aliye katika mahali pa siri; na Baba yako aonaye kwa siri, atakubariki kwa uwazi” (Mathayo 6:6).
Yesu anaposema juu ya kwenda mahali pa siri kumtafuta Baba, anasema juu ya kitu kikubwa sana kuliko kitu kinacho kuwa kalribu ya mwili. Anazungumzia mahali popote ambapo unaweza kuwa peke yake naye katika ushirika wa karibu.