Body

Swahili Devotionals

KUKIMBILIA MBELE YA MUNGU

Tim Dilena

Baada ya Yoshua kuchukua uongozi wa wana wa Israeli kutoka kwa Musa, aliwaongoza kwenye ushindi mkubwa - haswa, Yeriko na Ai. Wakati Mungu akifanya miujiza mingi ya kushangaza kwa Waisraeli, uongozi wa Yoshua haukuwa kamili bila ubaguzi mmoja mbaya. Wagibeoni wenye hila waliingiliana na kumshawishi afanye uamuzi bila kushauriana na Mungu juu ya hilo (ona Yoshua 9:3-13). “Ndipo watu wa Israeli walitwaa riziki yao; lakini hawakuuliza ushauri wa Bwana. Naye Yoshua akafanya amani nao, na akafanya agano nao” (Yoshua 9:14-15).

KUELEKEZA MACHO KWA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

"Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiaaga mkutano. Naye alipokwishwa kuwaaga mkutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.” (Mathayo 14:22-24).

TUNAKUWA KILE TUNACHOKIONA

David Wilkerson (1931-2011)

Stefano aliona mbingu zikiwa wazi na Mtu aliyetukuzwa kwenye kiti cha enzi ambaye utukufu wake ulionekana ndani yake kwa wote waliosimama karibu. "Lakini yeye, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akatazama mbinguni na kuona utukufu wa Mungu, na Yesu amesimama mkono wa kulia wa Mungu, akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguliwa na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kulia wa Mungu!'” (Matendo 7:55-56).

SAUTI KATIKA JANGWANI

David Wilkerson (1931-2011)

Yohana Mbatizaji alielezea huduma yake waziwazi na kwa urahisi aliposema, "Mimi ni sauti ya mtu aliaye jangwani" (Yohana 1:23). Mtumishi huyu wa yule Aliye Juu zaidi ambaye, kulingana na Maandiko, alikuwa mkubwa zaidi "kati ya wale waliozaliwa na wanawake" (Mathayo 11:11), alikuwa mtu bora zaidi, aliyebarikiwa sana na manabii wote na mhubiri aliyeheshimiwa wa haki.

ACHIA VITA MIKONONI MWA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

"Avikomesha vita" (Zaburi 46:9). Habari gani ya kukaribisha kwa ajili ya mtoto wa Mungu ambaye anapungukiwa na kung'olewa na vita. Vita katika roho yetu ni vita vyake, na yeye tu ndiye anayeweza kuimaliza. Baba yetu mwenye upendo hataruhusu mwili au ibilisi kutunyanyasa ili tushindwe.

KUJIANDAA KWA AJILI YA VITA

Gary Wilkerson

"Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kupitana hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya ufalme na mamlaka, juu yawa kuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho ... Kwa sala zote na maombi mkiomba kila wakati katika Roho" (Waefeso 6:10-12, 18).

MAHITAJI YA USHILIKIANO WA KIKRISTO

Jim Cymbala

"Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi yaw engine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia" (Waebrania 10:25).

Ni baraka kufanya ibada pamoja na waumini wengine. Kuimba nyimbo za Bwana, kusikia Neno lake la thamani linafafanuliwa, kuinua sauti zetu kwa sala pamoja na Wakristo wengine, kwa upendo na kupendwa - hizi ni njia ambazo Bwana hutumia kuimarisha mioyo yetu.

UNAPENDWA NA UNAKUBALIWA

David Wilkerson (1931-2011)

Yeremia alikuwa nabii mwenye moto mkubwa wa Agano la Kale. Kila neno alilohubiri lilikuwa kama upanga unaokata mwili. Alikasirisha wanasiasa na viongozi wa kanisa kiasi kwamba walimtupa gerezani.

Lakini wakati wote, nabii huyu analia alitazamia siku ambayo Mungu atatembelea watu wake na kubadili mioyo yao. Yeremia alijua ya kuwa Mungu alihurumia watu wake na aliwapenda kwa upendo wa milele.

KILIO KINAONGEZEKA

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu anataka kuvunja kupitia kwa watu wake. Kama maandiko yatabiri, ibilisi ameshuka kwa hasira kubwa, akijua kwamba wakati wake ni mfupi. Hivi sasa, watu wa Mungu wanahitaji kumiminwa mkubwa wa Roho Mtakatifu; kugusa kusiko kawaida kuliko ule wa Pentekosti. Kilio kinachoalikwa leo kilisikika katika siku za Isaya: "Laiti, ungepasuwa mbingu, na kushuka, ili milima itetemeke mbele zako … Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu hawatambui kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila Wewe, anayetenda mambo kwa ajili yake amngojea. (Isaya 64:1, 4).