Body

Swahili Devotionals

JE! UNAAMINI ULINDAJI WA MUNGU?

David Wilkerson (1931-2011)

Kuna wakati kunaonekana kama Mungu hajajidhihirisha - wakati watu wake wameachwa kwa aibu na kukata tamaa - lakini hadithi kamili bado haijaambiwa. Katika Bibilia yote Mungu amekuwa na watu ambao imani kama-marumaru ilithibitisha uaminifu wake wakati wa nyakati ngumu zaidi. Watumishi hawa, bila woga, walimuachia Bwana kutenda.

USIOGOPE KILE UNAONA

David Wilkerson (1931-2011)

"Maana mikono ya waovu itavunjika, lakini BWANA huwasaidia wenye haki ... Hawataaibika wakati wa ubaya" (Zaburi 37:17, 19). Utabiri huu wa kushangaza kwa watu wa Mungu unatimizwa mbele ya macho yetu. Zaburi ya 37 inatuambia kwamba Bwana anainuka kuchukua hatua dhidi ya jamii ambayo dhambi zawo zimefika hadi mbinguni. Ndio Zaburi hii hiyo ni mojawapo ya tumaini kubwa, iliyo na ahadi ya ajabu kwa wale wanaomtegemea kabisa Bwana.

NJAA YA NAFSI

David Wilkerson (1931-2011)

Kuna njaa mbaya ya kutisha katika nchi hii leo. Sio njaa ya chakula bali ya hitaji la wanadamu. Watu wengi sana wamekosa upendo na ushikamano; kwa amani na kuridhika; kwa kusudi na kutimiza. Kwa kweli neno la njaa linamaanisha" uhaba mkubwa, njaa isiyokamilika, njaa ya aina yoyote." Hiyo inaelezea vizuri utupu ambao wengi wanapata leo.

NJIA YA KUELEKEA USHINDI

Gary Wilkerson

"Tangu sasa musiendene kama watu wa mataifa waendavyo ... Sivyo mlivyojifunza Kristo ... na mkafundishwa ndani yake ... mjivue tabia zenu za zamani, ambazo ni za maisha yenu ya zamani… na kuvaa utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli” (Waefeso 4:17, 20-24).

NGUVU YA KUSHINDA MWILI

David Wilkerson (1931-2011)

"Na ile damu itakuwa ishara kwako katika nyumba mtakazokuwamwo; nami nitakapoiona ile dhambi, nitapita juu yenu, ili lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misiri” (Kutoka 12:13).

WEKA CHINI SANAMU ZAKO ZA MWISHO

David Wilkerson (1931-2011)

Jaboki, mahali ambapo Yakobo alipambana na Mungu na akajitolea kabisa, anaonyesha mahali Wakristo wanapigana vita vyao vya kibinafsi. Hakuna washauri, hakuna marafiki, hakuna wasaidizi - wewe tu na Mungu. Katika Yaboki Yakobo alitupa chini sanamu yake ya mwisho na akashinda ushindi wake mkubwa. Na hapo alipokea tabia yake mpya na jina lake mpya - Israeli.

KINACHOVUNJA MOYO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alilia kwenye kaburi la Lazaro ingawa alijua kuwa hivi karibuni angemfufua. Baada ya yote, alikuwa amekuja Bethania kwa kusudi hili. "Yesu akalia. Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda! Na wengine wao wakasema, Je! Huyu ambaye alifumbua macho ya kipofu, hakuweza pia kumzuia mtu huyu asife? akaja kaburini” (Yohana 11:35-38).

KUSHIKILIA USHINDI

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu hadharau watoto wake wakati anaahidi, "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale ambao wameitwa kulingana na kusudi lake" (Warumi 8:28). Na yeye sio mwongo wakati anaahidi, "Macho ya BWANA yako juu ya wenye haki, na masikio yake hukielekea kilio chao ... Wenye haki walilia, naye Bwana akasikia, na kuwaokoa katika shida zao zote" (Zaburi. 34:15, 17).

NYOKA KATIKA BUSTANI YAKO

Gary Wilkerson

"Mungu akaona kila kitu ambacho alichokifanya, na tazama, kilikuwa kzuri sana" (Mwanzo 1:31). Kwenye Mwanzo sura ya 1 na 2, tunasoma juu ya uumbaji mzuri wa Mungu. Adamu na Eva walishiriki ushirika mtamu na baba yao katika bustani ya Edeni - lakini pia kulikuwa na nyoka kwenye Bustani. "Basi nyoka alikuwa mjanja zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote wa shamba ambalo BWANA Mungu alikuwa ameumba" (Mwanzo 3:1). Kiumbe hiki chenye ujanja na chenye uwongo kilimjaribu Hawa, ambaye aliletea mumewe katika mpango huo, nao wakakubali sauti yake.