Body

Swahili Devotionals

KUJIFUNZA KUSIMAMA JUU YA NENO LA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mazoezi ya kubadilisha mara nyingi ni  wakihisia kwa sababu ni mpya na ya kipekee sana. Ni ajabu sana kuokolewa na dhambi na utumwa na kuingia katika maisha mapya mzima katika Kristo.

Ukuaji wetu wa kwanza wa kiroho ni kama mtoto anajifunza kutembea. Ni kusisimua wakati mtoto atachukua hatua zake za kwanza na kuna faraja nyingi na kufurahisha. Lakini baada ya kuanza kutembea, yeye si tena kituo cha tahadhari, na wakati anaanza kung’oa mimea na kula mahali pote ndani yanyumba, anapewa nidhamu, ingawa kwa upole, na vitu havisisimuwi tena.

"UKO WAPI?"

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo ambao wanashindwa kuomba hawatambui hatari waliyo nayo. Unaweza kusema, "Basi ni nini ikiwa Wakristo wengine hawaombi? Wao bado wanaamini - watasamehewa na kwenda mbinguni."

Baba yetu wa mbinguni anafahamu kama tunaishi wakati washuguli nyingi, na mahitaji mengi juu ya wakati na nguvu zetu, na Wakristo wamejipata katika shughuli na kazi nyingi kama mtu mwingine yeyote. Hata hivyo, siwezi kuamini Mungu kama anachukua sana ukataaji wetu kwakutomufikilia, ambayo ilimugalimu Mwana wake peke maisha yake.

KUOMBA KABLA YA MGOGORO

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati Yesu alipokuwa akitembea hapa duniani, alijihusisha na watu wote. Alifundisha katika masinagogi, juu ya milima na kwenye boti, akiponya wagonjwa na kufanya miujiza. Aliinua sauti yake kwenye sikukuu, akalia, "Mimi ni maji yaliyo hai! Njoo kwangu na nitamariza kiu ch nafsi yako." Mtu yeyote anayeweza kumkaribia na ataridhika. Lakini mwaliko wa Bwana wetu ulipuuzwa zaidi.

KUJIAMINI KWA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo wengi wanafahamu mstari huu: "Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi" (Waebrania 4:15). Tunaona hapa kwamba kuhani wetu mkuu, Yesu, anahisi mateso yetu pamoja nasi. Kwa maneno mengine, Bwana binafsi anaguswa na maumivu yote, kuchanganyikiwa na kukata tamaa tunayohisi. Hakuna kitu tunachokipitia kwamba hakukipitia pia, kwa njia moja au nyingine.

KUOMBA NA USIPOTEZE MOYO

Gary Wilkerson

"Akawambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. Akasema, palikuwa na kadhi katika mji Fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Nakatika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endeahaki akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mujane huu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima."'

JE, TUNA MIOYO YA HURUMA?

Nicky Cruz

Ikiwa tunataka kuwafikia watu kwa ajili ya Yesu, hebu tupate somo kutoka kwa mtume Paulo. Alijua jinsi ya kuwafikia watu kwa ujumbe wa wokovu.

Alipokuwa Athene, Paulo alisumbuliwa na idadi kubwa ya watu wanaabudu sanamu na miungu ya uwongo. Alijua jinsi ya kuingia katika utamaduni wao kwa undani sana na aligundua kuwa ili kuwafikia, alihitaji kupata imani yao. Alikuwa na muda pamoja na watu, kujifunza juu ya maadili na imani zao na kujiingiza ndani ya utamaduni wao.

BWANA, KWA NINI?

David Wilkerson (1931-2011)

Sio dhambi kwa muumini kuuliza kwa nini; hata Bwana wetu aliuliza swali hili alipokuwa akipigwa na maumivu msalabani (angalia Mathayo 27:46). Wakati mwingine tunaweza kulia, "Bwana, kwa nini unanipisha kwa njia hii? Najua haitoki kwa mkono wako, lakini bado unaruhusu shetani aendeleye kunisumbua. Je, ni lini hayo ataisha?"

"TUTAFANYA HILO KWA NIYABA YETU"

David Wilkerson (1931-2011)

Mtume Isaya alisema juu ya Israeli: "Ole wao watoto waasi; asema Bwana, watakao mashauri lakini hawataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha Roho yangu; wapate kuongezeka dhambi juu ya dhambi " ( Isaya 30:1). Neno la Kiebrania, ole hapa linamaanisha huzuni na maumivu juu ya kile ambacho Mungu anaelezea kama uasi, maana ya kurudi nyuma, ukaidi, kugeuka.

KUSONGA MBERE KARIBU NA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana anajitayarisha kumwaga Roho wake juu ya watu wake katika siku hizi za mwisho na najua unataka kuwa na sehemu ndani yake. Ili jambo hili lifanyike, lazima tuwe karibu na yeye - katika ibada yetu, utii na bidii. "Mkaribie Mungu naye atawakaribia ninyi" (Yakobo 4:8).