Body

Swahili Devotionals

JE! MOYO WANGU UMEBADILIKA?

David Wilkerson (1931-2011)

"Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imana; jithibitisheni wenyewe" (2 Wakorintho 13:5).

Neno la Kigiriki la "kujaribu" hapa linamaanisha "kuchunguza, tathmini." Mtume Paulo anasema, "Jaribio mwenyewe ili uone kama unatembea kulingana na Neno la Mungu." Tunapaswa kujiuliza daima, "Je, ninabadilisha? Je, nina upendo zaidi na moyo wenye huruma? Je! Mazungumzo yangu yanakuwa yenye haki zaidi? Je! Bado ninalalamika au ninaanza kuzungumza maneno ya imani? Je, ninajaribu kumpendeza Yesu?"

JE! UNAJUA KAMA KRISTO ANAISHI NDANI YA MOYO WAKO?

Gary Wilkerson

"Hamujui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la mungu, na kuwa roho wa Mungu anakaa ndani yenu?" (1 Wakorintho 3:16-17).

Paulo anaanza sehemu hii ya barua hii kwa kuuliza, "Je, hamujui?" Ni swali kidogo la kutisha kwa sababu Wakristo wa Korintho walikuwa karibu miaka minane katika imani yao, lakini anawauliza mojawapo ya msingi wa maswali . "Hamujui kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu?" Labda hawakuweza kuzingatia ukweli huo ingawa Paulo alikuwa amefundisha hapo awali.

MARAFIKI ZAKO NI WENYE MAANA KUBWA KWA MUNGU!

David Wilkerson (1931-2011)

Labda una marafiki wa aina mbalimbali wanaojumuisha ulimwengu wako wa kibiashara – watumishi wenzako, washirika au wateja - na marafiki unao ushirika kwa kiwango cha juu. Tunapaswa kuondoka ulimwenguni kabisa ili kuepuka aina hizi za mawasiliano.

Mungu anajali zaidi kuhusu mzunguko wako wa karibu, marafiki zako wa ndani. Hawa ndio watu unaowapenda zaidi na wanao ushawishi katika maisha yako. Unakubaliana juu ya vitu vingi na unasikia salama kufungua moyo wako kwa kila mmoja.

"USIOGOPE!"

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu ametuamuru tusiwaogope adui zetu. "Usiwaogope" (Kumbukumbu la Torati 7:18). Kwa Israeli, "wao" waliwakilisha uwingi wa mataifa wakipagani, yenye kujihami na silaha zenye nguvu ambayo walikabili katika Nchi ya Ahadi. Kwa sisi leo, "wao" inawakilisha tatizo lolote, shida na matatizo magumu tunayopata katika maisha.

Mungu anasema tusiogope, kwa hiyo hakuna maelezo mengine yanaohitajika. Mungu ni nguvu zote na anajua ngome za shetani tunazokabiliana nazo - kila mtego, magumu na majaribu. Lakini bado anasema, "Usiogope lolote kwa hao!"

UPENDO WA AJABU WA BABA

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo ambao ni muhimu kuhusu kutembea kwao na Mungu wana hamu kubwa ya kujua Baba yao wa mbinguni bora. Maandiko yanasema waziwazi, "Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote" (Yohana 1:18). Tunajua kwamba Mungu ni roho na yeye haonekani kwa macho yetu, basi tunawezaje kumjua Baba? Naamini sehemu moja ya kazi za Yesu hapa duniani ilikuwa kutufunulia uso wa kibinadamu wa Baba wa mbinguni.

KUTOJIFANYA KUWA MWENYE SIFA

Gary Wilkerson

Yesu alikuwa na moyo wa mtumishi na anatuita kufanya utumishi. "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayonilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; amabaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba" (Wafilipi 2:5-8).

Ninataka kukupa mambo sita ambayo Yesu anataka kutuambia leo kuhusu kutumikia:

FARAJA KWA MIOYO YETU YENYE HOFU

David Wilkerson (1931-2011)

Maisha ya Kikristo sio maisha yenye safari ya wazi kila wakati. Kila mwamini lazima apitie siku mbaya, bila kujali kwamba ni mtakatifu. Kwa kushukuru, Wakristo wengi wanatambua kwamba Yesu hayupo tu wakati mambo yanaendelea vizuri, lakini pia yupo na wakati wa magumu. Yeye ni mwaminifu na mwenye kujali kwa kila msimu na anaguswa na kila hisia tunayopitia.

NI NINI KINACHOONGOZA MAISHA YAKO?

David Wilkerson (1931-2011)

Leo wakristo wanaishi wakati wa mwanga mkubwa. Roho Mtakatifu ametufunulia maana yenye nguvu ya kazi ya Yesu msalabani, na baraka za ajabu hii ina maana katika maisha yetu. Hata hivyo kulikuwa na wakati ambapo kazi ya ajabu ya Kristo ilikuwa imefungwa kutoka ulimwenguni. Kipindi hicho kilijulikana kama Miaka ya Giza, kwa maana msalaba ulikuwa umefunikwa kutoka machoni ya ubinadamu.