KUSUBIRI AHADI KWA IMANI
Mungu anapowaambia wanadamu, “Amini,” anadai kitu ambacho hakina akili kabisa. Imani haina mantiki kabisa. Ufafanuzi wake unahusiana na kitu kisicho na akili. Maandiko yanatuambia, “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1). Tunaambiwa kwa ufupi, "Hakuna kitu kinachoonekana, hakuna ushahidi unaoonekana." Pamoja na hayo, tunaombwa kuamini.