Body

Swahili Devotionals

MUNGU ANA MPANGO KATIKA KAZI

David Wilkerson (1931-2011)

Mpendwa, ni muhimu kufahamu kama watu wengine wanaangalia maisha yako na kuathiriwa na tabia yako. Kwa hiyo, nauliza, Je!Unamwenendo gani katika tabia yako? Je! Watoto wako wamewekwa ndani Kristo kama wanavyoona mwenendo wako? Je! Wakristo wenye kiwango cha chini wanavutiwa kumjua vizuri zaidi kwa sababu ya ushuhuda wako? Je! Wenye dhambi wanavutiwa na Yesu kwa sababu ya majibu yako ya upendo? Unapokutana na changamoto katika kutembea kwako kwa kila siku, je! Una harakia kunyenyekea Roho Mtakatifu? Au je, wewe hulalamika na kumlaumu, na hatimaye kuwa kimya kwa Baba yako wa mbinguni?

DAMU YA YESU NI YA THAMANI KUBWA

David Wilkerson (1931-2011)

Bila shaka, damu ya Yesu Kristo ni zawadi ya thamani kubwa Baba yetu wa mbinguni ametupa. Wakristo walikuwa wakiimba juu ya nguvu za damu katika wimbo uliopendwa wa zamani ambao ulisema, "Kuna nguvu, nguvu, nguvu za kufanya kazi ya ajabu katika damu ya thamani ya Mwanakondoo."

Ninaogopa, hata hivyo, kwamba tunashindwa kuelewa umuhimu mkubwa wa damu ya Yesu. Wakati ni kweli kwamba kwa njia ya damu yake tunafunguliwa kutoka utumwa wa uovu - dhambi zetu zote zinafunikwa - kuna ukweli zaidi na maana katika thamani ya damu yake.

UTAJIRI WA SALA YA BWANA

Carter Conlon

Yesu anasema, "Utupe leo mukate wakila siku. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe  na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina" (Mathayo 6:11-13).

JE! UKO NDANI YA UPENDO PAMOJA NA YESU?

David Wilkerson (1931-2011)

"Kwa Imani Henoki lihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu" (Waebrania 11:5).

Henoki alimtii Mungu kwa lengo pekee la kumpendeza Mungu na alipewa thawabu na Baba kwa kutafsiriwa - inamaanisha kwamba alipelekwa mbinguni bila kufa. Yote kwa sababu alimpendeza Bwana!

"Na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake" (1 Yohana 3:22).

HAMU HALISI YA KUMPENDEZA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

"Na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyo nifundisha ndivyo ninenavyo. Naye aliye nituma yu pamoja name, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo." (Yohana 8:28-29).

Yesu alifanya kila kitu kutokana na radhi kwa Baba yake wa mbinguni. Ni muhimu kuelewa lengo ambalo utii wetu unapatikana, kwa sababu ikiwa moyo wetu si safi, kila kitu hakitastahili.

HALI YA MOYO

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo wengi husema, "Naam, mimi ni mwamini. Nimejenga juu ya Mwamba." Hata hivyo, hawajui maana ya neno hili, na watakuwa na mshtuko mkubwa wakati uhusiano wao na Yesu hauwezi kuvumilia dhoruba.