MUNGU ATAKUHIFADHI KUTOKA KWA ADUI

David Wilkerson (1931-2011)

"Wale wanaofuata njia ya uovu; wao ni mbali na sheria yako. Wewe u karibu, Ee Bwana, na amri zako zote ni kweli" (Zaburi 119:150-151, AMP).

Kuna ukweli wa utukufu katika kifungu hiki ambacho kinaweza kubadilisha maisha yako, kukuletea amani na kukupa kupumzika zaidi ya yoyote uliopitia. Unaona, mara tu unapoelewa ukweli usio badilika wa Mungu unakusogelea karibu yako - kwamba anakupenda na anaendelea kuwa karibu na wewe-hofu na wasiwasi lazima viende!

MUNGU ALIKUITA KWA JINA

David Wilkerson (1931-2011)

"[Bwana] akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami" (Zaburi 18:19).

Maneno mazuri, yenye kuhimiza. Baba hufurahia kwetu! Katika kesi ya Daudi, alikuwa amepita wakati wa kutisha. Sauli alikuwa ameweka fadhila juu ya kichwa chake na Daudi alikuwa akikimbia kwa ajili ya maisha yake. Lakini Mungu alikuja kwa ujasili ili kumwokoa naye na Daudi angeweza kusema, "Sababu Mungu aliniokoa kutoka kwa adui zangu wote ni kwa sababu mimi ni wa thamani kwake. Mungu wangu anifurahia mimi!"

WAKATI UPEPO UNAPO PINGANA NA SISI

Gary Wilkerson

Mtume Paulo alikuwa na kusudi la uhakika, maono, ujumbe - utume wa Mungu. Uzoefu wake wakipeke ulimfanya awe daima kwenda mbele. Alijua kwamba angeweza kukabiliana na shida nyingi, lakini alifundisha kwamba unaweza kuvumilia mateso mengi wakati moyo wako umewekwa kwenye malengo. Ikiwa moyo wako umewekwa kwenye faraja, hakuna mateso unaweza kuvumilia kamwe.

BABA MWENYE UPENDO ZAIDI

Jim Cymbala

Martin Luther, kuhani wa karne ya kumi na sita ambaye alianzisha Mapinduzi ya Kiprotestanti, alikuwa na hofu ya kwanza kwa Mungu, kwa sababu aliamini kwamba Bwana alikuwa hakimu mtakatifu lakini mwenye hasira - ambayo ndiyo ilikuwa wakati wakisheria za siku yake ilimfundisha kuamini. Haijalishi jinsi Martin alivyojaribu kumpendeza Mungu huyu mtakatifu, alishindwa, alihisi kuwa anahukumiwa na Mungu, na akahisi hatia ya dhambi yake.

MUNGU ANA MPANGO KATIKA KAZI

David Wilkerson (1931-2011)

Mpendwa, ni muhimu kufahamu kama watu wengine wanaangalia maisha yako na kuathiriwa na tabia yako. Kwa hiyo, nauliza, Je!Unamwenendo gani katika tabia yako? Je! Watoto wako wamewekwa ndani Kristo kama wanavyoona mwenendo wako? Je! Wakristo wenye kiwango cha chini wanavutiwa kumjua vizuri zaidi kwa sababu ya ushuhuda wako? Je! Wenye dhambi wanavutiwa na Yesu kwa sababu ya majibu yako ya upendo? Unapokutana na changamoto katika kutembea kwako kwa kila siku, je! Una harakia kunyenyekea Roho Mtakatifu? Au je, wewe hulalamika na kumlaumu, na hatimaye kuwa kimya kwa Baba yako wa mbinguni?

DAMU YA YESU NI YA THAMANI KUBWA

David Wilkerson (1931-2011)

Bila shaka, damu ya Yesu Kristo ni zawadi ya thamani kubwa Baba yetu wa mbinguni ametupa. Wakristo walikuwa wakiimba juu ya nguvu za damu katika wimbo uliopendwa wa zamani ambao ulisema, "Kuna nguvu, nguvu, nguvu za kufanya kazi ya ajabu katika damu ya thamani ya Mwanakondoo."

Ninaogopa, hata hivyo, kwamba tunashindwa kuelewa umuhimu mkubwa wa damu ya Yesu. Wakati ni kweli kwamba kwa njia ya damu yake tunafunguliwa kutoka utumwa wa uovu - dhambi zetu zote zinafunikwa - kuna ukweli zaidi na maana katika thamani ya damu yake.

UTAJIRI WA SALA YA BWANA

Carter Conlon

Yesu anasema, "Utupe leo mukate wakila siku. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe  na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina" (Mathayo 6:11-13).